NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Je Mzimu Wa Lowassa Utaibuka Kikao Cha CCM Dodoma?

Edward Lowassa.

Wakati CCM ikijiandaa kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti, suala la masalia ya Edward Lowassa linaweza kuchukua nafasi kubwa katika vikao vitatu vya juu vinavyofanyika kwa mara ya kwanza tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Mkutano Mkuu Maalumu ulio na ajenda moja tu ya kumchagua mwenyekiti mpya hautakuwa na nafasi ya kujadili ajenda nyingine, lakini Halmashauri Kuu iliyogawanyika baada ya Lowassa kuenguliwa kwenye mbio za urais, inaweza kuchukua muda kujadili CCM mpya baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kujiondoa Julai 28 mwaka jana.

CCM itaanzia mikutano yake kwa kikao cha Kamati Kuu, ambayo hufanya maandalizi ya kikao cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Ijumaa na kumalizia na Mkutano Mkuu Jumamosi wiki hii.

Pia kutakuwa na kikao kingine cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Jumapili ambacho kwa sehemu kubwa kinatarajiwa kujadili taarifa za wasaliti zilizoandaliwa na kamati za siasa za mikoa na huenda kikatoa maamuzi mazito yanayobeba mustakbali wa kuijenga “CCM ya Magufuli”.

Kada na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma ambaye awali mwaka jana aliweka wazi mahaba yake na kumuunga mkono Lowassa  amesema suala la masalia ya Lowassa kuibuka kwenye vikao hivyo amedai kuwa waliomuunga mkono mwanasiasa huyo maarufu walifanya hivyo wakati akiwa CCM na kwa kuwa hawakumfuata hawatarajii suala hilo kuibuka tena.
“Makundi ndani ya CCM yalikwisha baada ya Magufuli kupitishwa kukabidhiwa kijiti,” amesema
Msukuma, ambaye alifanya mbwembwe za kuhama kambi ya Bernard Membe kwa kutua na helikopta kwenye mkutano wa Lowassa mjini Arusha, alisema wakati CCM ikisaka mgombea wake wa urais, kulikuwa na makundi zaidi ya 40.
“Wakati ule kila mgombea alikuwa na kundi. Ila kwa sasa sidhani kama hali hiyo bado ipo maana baada ya mgombea kupatikana kila mmoja alimuunga mkono,” ameongeza Msukuma.
Majibu ya yote haya yatapatikana ndani ya siku chache zijazo ikiwa zimebaki siku mbili tu kwa Chama hicho kuanza michakato yake ya Mkutano wake Maalum ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda moja kubwa ya kumkabidhi Rais, Dkt. John Magufuli hatamu ya uongozi wa chama hicho Taifa kutoka kwa Mwenyekiti anayeondoka Dkt. Jakaya Kikwete.
Lowassa alikihama chama hicho na kuhamia CHADEMA baada ya jina lake kukatwa katika harakati za kugombea nafasi ya kusimamisha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana huku ikidaiwa kuwa
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment