Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali tamko
la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe
27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya
vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi
nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta
uvunjifu wa Amani.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha
Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi
imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya
Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha
siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya
kufikia malengo yake ya kisiasa.
“Nimepokea
kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari,
kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa
lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa
amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa
maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya
Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.
Aidha,
taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha
siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi,
kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea
uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa,
Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa
kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.
Nakuongeza
kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno
yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha
siasa chochote.
Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).
Natumia
fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya
Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze
tabia hii.
Jaji
Mutungi ametoa rai kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa waonyeshe ukomavu
katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au
matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na
Serikali yao.
Katika
tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni
siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo
ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.
0 comments:
Post a Comment