Mwana FA anatarajia kwenda tena nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo wake ujao.
Hiyo itakuwa video ya pili yake mwenyewe kuifanyia nje ya nchi baada ya ile iliyopita ya wimbo wake ‘Asanteni kwa Kuja.’
Akieleza sababu ya kurudi tena SA kufanya video yake, FA ameiambia
Bongo5, “Kitu cha kwanza ni ile professionalism yao, ni kama watu wako
very serious na kazi yao kiasi kwamba hawakupi pressure, mlichokubaliana
ndio kinakwenda hivyo hivyo.”
“Cha pili hata kama ni kufanya muziki ambao utaconquer Tanzania na
Afrika Mashariki kwasababu ndio soko ambalo mimi binafsi nalitolea
macho, lakini bado unataka kuwa na kitu ambacho unakionesha kwamba ‘huu
ni muziki wa nyumbani kwetu nimeufanya lakini naweza kumuonesha mtu
yeyote Afrika na mtu yeyote duniani kwamba hii ndio video nimefanya,”
ameongeza.
“Haimaanishi kwamba unataka kufanya video kwaajili ya Watanzania
ufanye fanye tu kwasababu unajua viwango vyetu vilipo yaani unashindana
na miguu yako mwenyewe, sio sahihi. Tunaangalia dunia inavyokwenda, kasi
yake na viwango vimeshapandishwa.”
FA anaamini kuwa kwa miaka yote 14 ambayo amefanya muziki video yake
ya mwisho ndio bora zaidi na hicho ndicho kitu kilichomfanya aamini
katika kusafiri kwenda kufanya video Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment