Producer Maximizer ambaye ametayarisha wimbo wa Aiyola wa Harmonize amefunguka sababu za yeye kutokuwa chini ya Label ya WCB inayomsimamia msanii huyo kama watu wengi walivyotarajiwa.
Akizungumza kwenye moja ya mahojiano yake na Planet Bongo Maximizer amedai kwamba label hiyo haikuweza kutimiza vigezo vya mkataba ambao yeye alikuwa anautaka.
“Unajua mimi ni producer ninayejielewa,sitaki nifanye nyimbo halafu mwisho wa siku unabaki tu kama ulivyo,kuhusu Wasafi kuna mikakati(ya kwenye mkataba) ambayo mimi niliwapa ambayo ni siri kidogo,mwisho wa siku nikashindwana nao lakini nikawaambia kama kuna kazi yoyote kutoka Wasafi nitaifanya ndio maana sasa hivi nafanya nao project nyingi tu” alifunguka Maximizer.
0 comments:
Post a Comment