Mnamo
mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa
notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Aidha,
taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao
na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha
notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia
hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba
kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao
hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Zoezi
hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za
waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa
kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo
basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na
waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi
ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza
majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
0 comments:
Post a Comment