Katika michezo kuna vitu vingi haswa
katika magoli kuna kitu kinaitwa ‘hat-tricks’ yaani mchezaji kufunga
magoli matatu kwa mchezo mmoja na zawadi yake kuondoka na mpira uliokuwa
unatumika katika mchezo huo, ili kutoa thamani kwa mfungaji.
Sheria hii ni nzuri mno haswa kutoa
hadhi kwa kufunga magoli matatu, maana sio rahisi kufunga magoli 3 kwa
mchezo mmoja, hivyo waliotunga sheria hii wanatakiwa wapongezwe kwa
kuangalia thamani katika michezo. Zifuatazo ni ‘hat-tricks’ zilizofungwa
kwa dakia chache. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi peke yao ndio
wanaweza kufunga ‘hat-tricks’ kwa furaha tu ila mchezaji wakawaida kazi
ngumu.
1. ANDY CARROL
Mchezaji wa zamani wa vilabu vya
Newcastle United, Liverpool na sasa Westham United aliifunga Arsenal
mwaka 2016 kwa kutumia dakika 7 ambapo mchezo huo umeisha kwa Arsenal
kuambulia sare ya 3-3.
2. Matt Mousillou
Mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa yeye amefunga hat-tricks kwa kutumia dakika 4 katika ushindi wa magoli 8-0 mwaka 2005.
3. Davida Villa
Huyu mchezaji wa zamani wa Barcelona kwa
sasa anacheza MSL Marekani, ameweka rekodi yake mwenyewe hadi leo hii
hakuna aliyoivunja amefunga magoli 3 kwa dakika 4 mwaka 2005-2006
wakati huo anacheza Valencia.
4. Robert Lewandowski
Amefunga magoli 5 kwa dakika 8 na hakuna
aliye ivunja rekodi hiyo kwa ligi ya Bundasliga mwaka 2015, pia
amefunga magoli 3 kwa dakika 3 mwaka huo huo na mchezo huo huo kipindi
cha pili.
5. Sadio Mane
Kwa sasa ni mshambuliaji wa Liverpool
alifunga magoli 3 msimu wa 2015-2016 akiwa Sauthampton rekodi yake
hakuna aliyeivunja kwani alifunga magoli 3 ndani ya dakika 3 yaani
13,14,15 dhidi ya Aston Villa.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WACHEZAJI WALIOFANIKIWA KUFUNGA MAGOLI MATATU KWA DAKIKA CHACHE
Reviewed by Newspointtz
on
11:34:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment