NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

NAHODHA AWAPA TAHADHARI CCM UCHAGUZI 2020

nahodha

 

WAZIRI Kiongozi mstaafu Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kitakabiliwa na ushindani mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulikoni ule wa mwaka jana.

Nahodha alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na watendaji wa CCM Jimbo la Amani katika Tawi la CCM kwa Wazee Sebleni, akiwa katika ziara ya kukutana na watendaji wa majimbo akiwa mlezi wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi.

Shamsi alisema uchaguzi ambao matokeo yake yalifutwa ulikuwa na ushindani mkubwa kati ya CCM na CUF na kuwataka viongozi na watendaji kufanya matayarisho mapema ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Alisema CUF walijiandaa zaidi na kufikia kufanya vitendo vya udaganyifu na kusababisha uchaguzi kuvurugika na kufutwa matokeo ya uchaguzi huo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

“CUF watajiandaa zadi kuliko kipindi kilichopita. Kama walifanya ghiriba mara tatu watafanya mara 10 zaidi, hivyo lazima tuwe na mipango na mikakati katika kuelekea uchaguzi mkuu,” alisema.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

1 comments:

  1. Nahodha ,maneno yake ni sawa na panga linalokata huku linajijuan linaumia enyewe
    huo ndio ukweli wenyewe

    ReplyDelete