NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Picha: Bintiye Obama akifanya kazi mgahawani

Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha ‘starehe’ za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
080316sashace002-1
Binti huyo wa umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts.
080316sashace002-1 (1)
Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
080316sashace005-1
Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.
Picha zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
080316sashace010
080316sashace014
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani.”
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment