JESHI
la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu
Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
baada ya kumaliza kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi.
Baadhi
ya viongozi waliofika kumwekea dhamana ni pamoja na Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Edward Lowassa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa
kamati kuu wa Chama hicho, aliyefika saa 12:14 jioni akiungana na
viongozi na wanachama wa chama hicho.
Baada
ya kufika Lowassa wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya
ofisi hizo za polisi walianza kuimba wimbo wa kumuita rais, rais, rais
ikiwemo na kauli mbiu ya maarufu ya Peoles power.
Mara
baada ya kufika alipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
aliyekuwa amepanda gari moja na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob
waliokuwa nje ya geti.
Viongozi
hao waliokuwa nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani na polisi waliongozana
na Lowassa kuomba kuingia lakini walizuiwa hali iliyofanya wachukue
uamuzi wa kuondoka.
Kiongozi aliyeruhusiwa kuingia alikuwa ni Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Akizungumzia
kuhusu hilo, Peter Kibatala mwanasheria wa Lissu alisema kwamba
mahojiano kati ya jeshi hilo na mtuhumiwa yalianza saa 9:30 hadi saa
12:30.
“Katika
maelezo ya polisi wanasema kwamba wakati Lissu akitoka mahakamani juzi
kwenye kesi yake alitamka maneno ya uchochezi, lakini haya yote
yanahitaji ushahidi,” alisema Kibatala.
Wakili
huyo alisema kwamba polisi baada ya kumaliza mahojiano na wao wakiwa
wameandaa utaratibu wa dhamana walikataliwa hadi leo Ijumaa
atakapofikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment