MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuanza kutembelea nyumba hadi
nyumba kuhakiki gharama za upangishaji ili kukokotoa na kukusanya kodi
sahihi ambayo ilikuwa haifiki serikalini. Hivyo, wamewataka wananchi
kutunza kumbukumbu za mikataba ya pango ili itakapohitajika na maofisa
wa mamlaka hiyo wawapatie.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
wakati akielezea kuhusu makusanyo ya kodi kwa mwezi Julai, Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema hatua
hiyo ni moja ya mikakati ya kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Alisema
kwa Julai, TRA imekusanya Sh trilioni 1.055 sawa na asilimia 95.6 ya
lengo la kukusanya Sh trilioni 1.103 iliyopangiwa na serikali kwa mwezi
huo.
Alisema ikilinganishwa na kipindi kama
hiki kwa mwaka jana, TRA ilikusanya Sh bilioni 914 ikiwa ni ongezeko la
asilimia 15.43 ya makusanyo ya mwezi huu huku kwa mwaka wa fedha
2016/2017, TRA imepewa lengo la kukusanya Sh trilioni 15.1
ikilinganishwa na lengo la mwaka jana la Sh trilioni 13.32.
“Natoa wito kwa wapangaji na
wapangishaji kujiepusha na aina yoyote ya udanganyifu katika suala zima
la kodi halisi ya pango kwa kuwa inaweza kuwasababishia kushtakiwa
endapo udanganyifu huo utabainika,” alieleza Kayombo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment