Baada ya ligi kadhaa kuanza barani Ulaya, yameanza kuibuka maswali
kuhusu uwepo wa Farid Musa nchini ikiwa awali iliarufiwa kwamba kinda
huyo wa Azam FC amefanikiwa kufuzu majaribio yake kwenye klabu ya
Tenerife ya nchini Hispania.
Klabu ya Tenerife iliridhia kumsajili Farid lakini kuna maswali mengi
yamezuka baada ya nyota huyo kuendelea kuonekana nchini huku baadhi ya
ligi zikiwa zimeshaanza kupigwa.
Sports Extra ya Clouds FM ilimtafuta Farid kwa ajili ya kupata
ufafanuzi wa jamo hili kwa kina zaidi na kipi kinachokwamisha yeye
kwenda Hispania hadi sasa.
“Taarifa niliyopewa na uongozi wa Tenerife ni kwamba, kila kitu
wameshawasilisha Azam na wamemalizana kwa kila kitu kwahiyo ni jukumu la
Azam kumaliza mambo yao na mimi namalizia baadhi ya mambo ubalozini,”
amesema Farid wakati akizungumza na kituo hicho cha radio.
Kuhusu yeye kutofanya mazoezi ya maandalizi ya pamoja na timu kwa
ajili ya msimu mpya, Farid amesema hiyo sio changamoto kubwa kwasababu
bado anaendelea kujifua na kujiweka fit wakati wote.
“Mchezaji ni kujielewa, mimi najua kitu gani nafanya na nini nataka.
Sibweteki tu nyumbani, naendelea kufanya mazoezi na Azam wakati mwingine
nafanya mazoezi yangu mwenyewe ilimradi kuweka sawa kiwango changu.”
“Kwasasa bado nipo chini ya Azam na bado wananilipa mshahara kama kawaida,” alimaliza Farid.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba amesema kila
kitu kinakwenda sawa na tayari wameshasaini mikataba ya Farid kuihama
Azam kwenda Tenerife na vimebaki vitu vichache tu kukamilisha dili hilo.
“Mikataba yote ya yeye kuhama kutoka Azam kwenda Tenerife
tumeshasaini, sasahivi Tenerife wanataka kuoiomba ITC yake ambayo ndiyo
tunamalizia kuikamilisha na ndani ya siku chache wataiomba na wataipata
halafu watatuma tiketi yake halafu Farid ataondoka,” amesema Kawemba.
“Mashabiki wa mpirwa wa Tanzania waelewe kwamba Farid si mchezaji wa Azam kwa sasa na anaondoka wakati wowote.”
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment