Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameshitushwa
na taarifa za tukio la tetemeko kubwa ardhi lenye mtikisiko wa kipimo
cha Ritcher 5.7 lililotokea Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya
Kanda ya Ziwa kadhalika nchi za Burundi na Uganda.
Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa mujibu wa taarifa ni
Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 10 na
wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa majengo mbalimbali.
Rais Malinzi mara moja anaungana na Serikali katika kusubiri tathmini
na kisha kuangalia namna TFF itakavyoweza kusaidia kama sehemu ya wadau
katika jamii. TFF inaamini kuwa baadhi ya waliopata maafa ni familia ya
mpira wa miguu si ndani tu ya nchi, bali pia nje ya mipaka ya Tanzania.
Hivyo, Rais Malinzi ametutuma salamu za rambirambi kwa familia zote
zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe
mahali pema peponi. Amina. Na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo
wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Katika salamu hizo, pia Rais Malinzi amemtumia Rais Shirikisho la
Mpira wa Miguu Burundi (BFF), Marlon Kuylen kwa sababu sehemu ya
Bujumbura imeguswa na tetemeko hilo kadhalika ametuma salamu za
rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Moses
Magogo baada ya ripoti kuonesha kuwa tetemeko hilo limeukumba mji wa
Kampala na Rakai nchini Uganda. Wataalamu wa elimu ya miamba – Jiolojia
wanasema kwamba lilikuwa ni kubwa kwa mujibu wa vipimo.
Home / News
/ Jamal Malinzi atuma salamu za pole kwa walio patwa na tukio la tetemeko kubwa la ardhi Mikoa ya Kanda ya Ziwa
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment