MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani
Katavi imewahukumu wakazi wa mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda, Godfrey
Mabuga na Rashid Ramadhani, kifungo cha miaka 20 jela.
Wamepewa adhabu hiyo baada ya
kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye
thamani ya zaidi ya Sh milioni 48 .
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki
na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga
Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka
huku ikimwachia huru mshtakiwa wa tatu.Baada
ya kusomewa hukumu hiyo, Mabuga na Ramadhani waliangua kilio mahakamani
hapo huku mshtakiwa aliyeachiwa huru akipiga magoti na kuonesha ishara
ya msalaba.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ntengwa
alisema mahakama hiyo imewatia hatiani watuhumiwa hao kupitia Kifungu
Namba 86 (1) na (2) cha Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009 na Kifungu
Namba 57 (1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka
2000.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
JELA MIAKA 20 KWA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO
Reviewed by Newspointtz
on
09:12:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment