Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania
Bara, Sebastian Nkoma amesema kwamba anakwenda Uganda kwa lengo moja
tu, kurejea nchini Tanzania na taji la Afrika Mashariki katika michuano
inayoratibiwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA.
Mara baada ya kambi ya kwenda uwanjani na kurudi majumbani kuanzia
Septemba mosi, nyota wa timu hiyo ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu
kwa jina la Kilimanjaro Queens, wameondoka kwenda moja kwa moja Bukoba
mkoani Kagera ambako itafanya kazi ya siku nne kuanzia Septemba 10,
2016.
Katikati ya kambi hiyo, Kilimanjaro Queens inatarajiwa kucheza na
Burundi ambayo pia itakuwa njiani kwenda jijini Jinja, nchini Uganda.
Burundi na Tanzania ambazo ziko makundi tofauti, zitacheza mchezo huo wa
kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Septemba
7, mwaka huu.
Michuano ya CECAFA ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati
itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.
Kwa mujibu wa CECAFA, Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango
vya Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa
pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za
Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda,.
Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12,
2016 kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia
zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa
kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.
Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya
zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza
na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga
hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.
Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika
Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na
nne.
Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya
kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka
la wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa
kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani
kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa
safari ya Uganda.
Home / Sports
/ Kocha wa Kilimanjaro Queens tuna kwenda Uganda kwa lengo moja tu kurejea nchini Tanzania na taji
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment