Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job
Ndugai amesema anampongeza Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa
namna ambavyo aliongoza bunge la bajeti ambalo lilidumu kwa siku 70
wakati ambapo yeye muda mwingi alikuwa kwenye matibabu nchini India.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa maswali
na majibu katika mkutano wan ne wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Spika Ndugai ametumia fursa hiyo kuwashukuru wabunge na
umma kwa namna walivyomwombea akiwa kwenye matibabu na hatimaye kurejea
salama.
“Ninampongeza
Naibu Spika kwa namna alivyoongoza Bunge akishirikiana na viongozi
wengine, kazi aliyofanya ni ya kupigiwa mfano kwa bunge lililodumu kwa
siku 70 kuanzia April 19 hadi Juni 30 mwaka huu” Amesema Ndugai.
Aidha Spika Ndugai amewataka wabunge
wote wa Bungen la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikiana katika
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kibunge.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
NDUGAI- DKT TULIA NI MWANAMKE SHUPAVU
Reviewed by Newspointtz
on
07:50:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment