NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

NILIPATA NAFASI PEKEE YA KUIFUNGA AZAM – KICHUYA

img_0068
Baada ya kufunga goli pekee lililoipa Simba pointi tatu dhidi ya Azam FC, Shiza Ramadhani Kichuya amesme, aliona ile ndiyo ilikuwa nafsi pekee ya yeye kufunga goli ukizingatia kocha wake Joseph Omog amekuwa akiwaelekeza wakipata nafasi nje ya 18 basi wajaribu kufunga.

“Kocha anatufundisha tukipata nafasi nje ya 18 tupige kwahiyo mimi nilipata nafasi nikaona ile ndiyo nafasi pekee nikapiga bahati nzuri nikafunga goli”, amesema Kichuya ambaye tayari ameifungia Simba magoli mawili kwenye ligi baada ya kucheza mechi tano.

“Najisikia faraja sana kwasababu kila siku napambana ili niwe nafunga magoli, nafurahi kufunga kwenye mchezo dhidi ya Azam na ntazidi kupambana ili niweze kufunga kwenye mechi zijazo.”

“Ushindi dhidi ya Azam umetufanya tuongoze ligi kwa kufikisha pointi 13, nafasi ya ubingwa ipo kila kitu kinawezekana na sisi tumekuja kupambana kuipatia mafanikio timu yetu.”

Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amekuwa na mchango mkubwa tangu aliposajiliwa Simba akiwa ameshacheza kwenye kikosi cha kwanza mechi zote tano ambazo klabu yake imecheza msimu huu.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment