Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kumpa pole kufuatia vifo vya watu na madhara mengine yaliyotokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Tetemeko
lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, limesababisha vifo vya watu 16,
kuacha watu 253 wakiwa na majeraha mbalimbali ya mwili na nyumba zaidi
ya 1000 zikiwa zimebomolewa.
Taarifa
kutoka kwa msemaji wa Rais Kenyatta alisema kuwa Rais Kenyatta ameahidi
kutoa msaada wa mabati, blanketi na magodoro ili kuwasaidia watu wasio
na makazi mkoani Kagera.
Msaada
huo utasafirishwa kwa ndege na Jeshi la Kenya Jumanne hii Septemba 13
hadi mkoani Kagera ambapo ndipo palipopata madhara.
Katika
hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jana aliwasili
mjini Bukoba kuwatembelea waathirika na kutoa mkono wa pole kwa kaya 16
za waliofikwa na misiba kutokana na tetemeko hilo la ardhi.
Mbowe
alitoa shilingi milioni 2.1 kwa ajili ya kaya hizo, mifuko 150 ya
sementi kwa familia 15 ambazo zimepoteza makazi ambapo kila kaya ilipata
mifuko 10.
Mwenyekiti
huyo wa Chadema aliambatana na viongozi wengine wa Chadema mjini humo
pamoja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Willfredy Rwakatale na Mbunge wa viti
maalum (CUF), Saverina Mwijage, walitoa sukari sukari kilo 25 pamoja na
mchele kilo 50.
“Ndugu
zangu, tukio hili sio la Serikali au chama chochote, ni jambo la
kitaifa. Serikali inapaswa kutenga fungu kubwa kwa ajili ya kuisaidia
jamii,” Mbowe anakaririwa.
Akiwa
katika shule ya Sekondari ya Ihungo iliyobomolewa na tetemeko la ardhi
na kusababisha wanafunzi kukosa madarasa ya kusomea, Mbowe ambaye pia
alisoma katika shule hiyo alitoa misaada mbalimbali.
Rais
John Magufuli alilazimika kuahirisha safari yake ya kuhudhuria
kuapishwa kwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu kutokana na janga la tetemeko
la ardhi, badala yake alimtuma Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
kumuwakilisha.
0 comments:
Post a Comment