NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Rooney aweka rekodi mpya timu ya taifa ya England

Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney ameweka historia ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu hiyo mara nyingi zaidi.
37E7735B00000578-0-image-a-25_1473006637573
Huu ulikuwa ni mchezo wake wa 116 kuiwakilisha England ilipokutana na Slovakia katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2018.

David Beckham ndiye alikuwa anashika rekodi hii kwa kucheza mechi 115 lakini kwasasa Rooney ameipita hiyo ya Beckham na kuandika yake ya kucheza mechi 116.

Mlinda mlango Peter Shilton, ndiye anaishika rekodi ya jumla kwa kuichezea England mara 125.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment