NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

SANCHEZ APIGA GOLI NA KUIOKOA ARSENAL KUFUNGWA NA PSG CHAMPIONS LEAGUE


1jAlexis Sanchez ameiokoa Arsebal kupoteza mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG baada ya kufunga goli dakika ya 78 kufuatia kupiga shuti kali lilitokana na kipa wa PSG

Alphonse Areola kuokoa mchomo uliopigwa na Alex Iwobi. Mchezo huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris maskani mwa PSG.

Edinson Cavani ndiye alifungua ukurasa wa magoli baada ya kuifungia PSG goli la mapema kabisa mnamo dakika ya 1 kwa kichwa safi na kuipa PSG goli la kuongoza

Kama si uzembe wa Cavani basi leo angeweza kufunga hat-trick kabla ya hata ya kwenda mapumziko lakini kazi nzuri ya David Opsina ilizuia magoli hayo.

Sanchez alipiga shuti lake la kwanza lililolenga lango dakika ya 12 kabla ya mchezo na kuisawazishia Arsenal bao hilo.

Alex Iwobi angeweza kuipatia Arsenal bao la pili lakini mpira uliokolewa na kipa wa PSG.
Olivier Giroud wa Arsenal na Marco Verratti wa PSG walitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufanyiana vitendo visivyo vya kiuanamichezo.

Dondoo muhimu za kufahamu

  • PSG wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 40 iliyopita waliyocheza katika uwanja wao wa nyumbani katika Michuano ya Ulaya (ushindi mara 25 sare 14).
  • Olivier Giroud ametolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye misimu miwili mfululizo.
  • Alexis Sanchez amefunga mara nne na kutoa assits tano kwenye mechi 14 za mwisho za Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa (64%).
  • Arsenal wameshindwa kupata ushindi kwenye mchezo hata mmoja kati ya mitatu iliyopita kwenye mechi za ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa hatia ya makundi (sare 1, kufungwa mara 2).
  • Goli la Edinson Cavani ni goli la mapema zaidi kwa Arsenal  kufungwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (sekunde ya 42).
  • Arsenal wamefanikiwa kutopoteza michezo 13 ya ugenini dhidi ya timu za Ufaransa kwenye Michuano ya Ulaya (ushindi mara 8 sare mara 5).
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment