Timu ya Serengeti Boys ya vijana chini ya umri wa miaka 17 imepata
ushindi wa mabai 3-2 dhidi ya Congo Brazzaville katika hatua ya tatu
kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani
AFCON 2017 Madagascar.
Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Yohana Mkomola aliyefunga
mawili na Issa Makamba, wakati magoli ya Congo yalifungwa na Langa Percy
kwa mkwaju wa penati na Bopoumela Chardon.
Mgeni rasmi alikuwa ni Nape Nnauye ambaye ni waziri wa utamaduni na
michezo aliahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha
hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake
itakuwa Sh 5,000,000. Kuna wabunge na viongozi wengine waliahidi kutoa
fedha zaidi.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2 ambapo mshindi wa hapo
atasonga mbele kwa kufuzu moja kwa moja katika michuano hiyo ya vijana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment