Baada ya msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele
kumuondoa Professor J katika list ya wasanii wa muziki wa hip hop baada
ya kushirikiana na msanii wa Singeli kwenye wimbo ‘Kazi Kazi’, Professor
ameamua kufafanua kwanini aliamua mshirikisha msanii wa kisingeli
kwenye wimbo hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Jumatatu hii, Afande Sele kupitia kipindi
cha XXL cha Clouds FM, kudai amekubali alichofanya Professor J kwenye
wimbo ‘Kazi Kazi’ lakini amemuondoa msanii huyo katika list ya wasanii
wa hip hip baada ya kukiuka miiko ya muziki huyo.
“Professor Jay ni mwanasiasa, mjanja, mwerevu, mwanasiasa anatakiwa
awe vile. Jay amesoma alama za nyakati, amefanya kitu ambacho wananchi
wake wa Mikumi ambao wamempa kura wanapenda. lakini kisanii kuna watu
amewakwaza, kwasababu bahati mbaya hip hop haiishii kwenye muziki tu,
hiphop ni utamaduni, kuanzia mavazi, maongezi na kila kitu.
Lakini aina
ya muziki ambao kafanya ni muziki flani ambao una upotoshaji kwa
maadaili ya hiphop, mambo kama kuserebuka, kumwaga razi na vitu kama
hivyo. Hicho ndio kimewakwaza watu wa hiphop. Lakini kwangu mimi
namchukulia kama mwanasiasa na amefanya kitu ambacho siasa inamtaka
kufanya.
Na Jay sasa hivi tumtazame kama mwanasiasa na sio mwanahiphop,
tukisema ni mwanahiphop tutakuwa tunamkosea sana.” Afande alikiambia
kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Kauli hiyo ilimvuta Professor J na kuamua kuzungumzia suala hilo ambalo imewagusa wasanii wengi wa muziki wa hip hop nchini.
“Kwanza nimshukuru sana Afande Sele kwa kuzungumza vizuri kwa mapana
na maono yake, naheshimu sana maono yake lakini mimi kitu kikubwa
ambacho naweza nikawaambia Watanzania ni kwamba sababu kubwa yakufanya
wimbo wangu wa sasa ‘Kazi Kazi’ na umefanya vizuri, nikutaka kufanya
jambo lingine tofauti.
Kwa sababu nimeshafanya kila kitu katika hip hop
na watu watakuwa mashahidi. Haya mapinduzi kwenye muziki yamechangiwa
sana na Professor Jay, kuwashawishi watu wazima kuona muziki wa hip hop
sio uhuni ingawa kuna wahuni wachache wanafanya muziki.
Lakini kitu
kikubwa ambacho nimejaribu kufanya mimi ni kiongozi, na kiongozi
unatakiwa kuonyesha njia kwa wale walio katatamaa.
Kama ambavyo
nilivyofanya mapinduzi kwenye bongofleva na kuufanya muziki wa
bongofleva kuweza kusikika na kuheshimika, nimeona kuna fursa nyingine
zipo kwenye muziki wa aina nyingine pia mchango wangu unatakiwa,”
Professor J alikiambia kipindi cha Amplifanya cha Clouds FM.
Alifafanua zaidi, “Pamoja kwamba mimi ni kiongozi na ni mbunge wa
jimbo la Mikumi lakini pia ni mwanamuziki na pia bado naendelea
kuangalia njia ya kufanya mapinduzi katika sehemu nyingine, mfano kwenye
muziki wa singeli naona kuna vipaji kabisa, naona kuna watu ambao
wanaweza wakafanya kitu ambacho kikasaidia kwenye ajira zao.
Kwa hiyo
nikaona kama kiongozi sio kitu kibaya kuwatengenezea njia ambayo
itawasaidia wao maana Professor J akifanya kitu watu wengi watakiona,
ndio maana sasa hivi hata Cholo Mwamba yupo busy na show mikoani, hicho
ndo nilichokuwa nataka kukifanya.
Lakini bado nimeendelea kubaki pale
nilipo, ndio maana nimechana kwenye beat ya Singeli, najua napenda
kufanya kitu ambacho mimi nakipenda mwenyewe kwa sababu mimi ni shabiki
namba moja wa muziki wangu, lakini najua kuna wengine nitakuwa
nimewakwaza.
Lakini niwaambie tu wasanii wengine wa hip hop pamoja na
mashabiki wa hip hip ambao nitakuwa nimewakwaza, umefika muda sasa
wakufanya mambo mengine katika hali ambayo ipo kwenye game, tuache
kwenda kwa kukariri kwamba hip hip ni hivi na hivi no, tunatakiwa
tufanye kazi katika kiwango chakutosha, kupitia muziki wa singeli ambao
unapendwa sana mtaani, nikaona nipenyeze ujumbe wa kuwaambia wafanye
kazi, waache kujiuza, waache kuuza madawa, waache kuvuta bangi, wafanye
kazi kwa bidii itawasaidia katika maisha yao.,”
Pia rapper huyo amesema ataendelea kufanya muziki wa hip hop katika kiwango cha juu zaidi.
Home / News
/ Baada ya Afande kumuondoa Professor J kwenye list ya wasanii wa hip hop kisa Singeli, Professor J aongea la moyoni
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment