Muziki ulimvuta Nick wa Pili aufanye kwakuwa yeye hakuwa na habari nao kabisa.
Rapper huyo amedai kuwa hata wimbo wake wa kwanza redioni ulitoka bila yeye kupanga.
“Mimi ni mtu ambaye sikuwahi kustruggle kurekodi au kutafuta kutoka.
Hata wimbo wa kwanza kusikika redioni ulikuwa ni by default,” Nick wa
Pili alieleza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.
“Nilikuwa natoka Mwenge naenda Mabibo and then Joh Makini alikuwa
anaenda all the way studio, tulivyofika pale river side akasema ‘hebu na
wewe tembelea studio uone kinatokea nini.’
Wakati yeye anaandaa verse
zake pale, mimi nikawa nimeingia booth nikawa kama nafreestyle yaani
kupass time. And then nilipotoka nikakuta watu wote kule studio wakiwa
wamesimama, walikuwa wamerekodi zile freestyle, so they want to keep it
iwe verse.
Nikasema ninaweza kufanya kingine zaidi ya hicho,” aliongeza.
“So from there pressure ya marafiki na nini na mafans nilikuwa nimeshapata so ikabidi niendelee.”
Katika hatua nyingine Nick alikiri kuwa kwa upande wa kipaji ukiwalinganisha na Joh Makini, kaka yake anamzidi mbali.
“Joh Makini ana experience kuliko mimi halafu naweza kusema in terms
of music yeye ana ujaribu mkubwa kuliko mimi, yeye amethubutu vitu vingi
ambavyo naweza kusema mimi baadaye nikaweza kufaidika kupitia hivyo
vitu. Nadhani Joh Makini will all due respect talent wise amenipita
mbali kwa mimi ninavyotizama.”
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment