NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

PAPA AMTUNUKU MTANZANIA TUZO YA HESHIMA

 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amemtunuku tuzo ya heshima ya mfano mwema Mtanzania, Janeth Mhella kutokana na utumishi uliotukuka.

Mhella amekuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo na Papa Francis, kutokana na  kumtumikia vyema kiongozi huyo na kanisa kupitia kazi aliyoifanya kwenye kituo cha redio.

Taarifa iliyotolewa jana, ilieleza tuzo hiyo ya juu na ambayo mtu hawezi kuipata kwa urahisi ilitolewa Alhamisi iliyopita na Kiongozi wa Sekretarieti ya Mawasiliano ya Ofisi ya Papa, Monsinyori Dario Vigno. Pia, watumishi wengine watano walitunukiwa tuzo na sekretarieti hiyo.

Tuzo hiyo kwa Kiitaliano inaitwa ‘Pro Ecclesia et Pontifice’ yaani medali ya Latini na kwa Kiswahili fasaha ni medali ya kanisa na Papa. Tuzo hiyo ya Kanisa Katoliki ilianzishwa na Papa Leo wa 13 mwaka 1888.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment