Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro, Stamina amesema hawezi
kwenda kushoot video nje kwa pesa nyingi wakati anaingiza pesa kidogo
katika muziki wake.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa muziki ni biashara kama biashara nyingine ambayo inazingatia faida na hasara.
“Muziki ni biashara na biashara kinachoingia ndicho unatakiwa
ukitoe,” alisema Stamina “Huwezi ukawa kwa mwezi unaingiza milioni 2
halafu ndani ya mwezi unatumia milioni 30. Hiyo ni hasara, namaanisha
kinachoingia kiwe sawa sawa nakinachotoka,”
Aliongeza, “Lakini mimi sasa hivi naona muda bado kutokana na bajeti,
kwa sababu mimi ni msanii ambaye toka naanza muziki sijawahi kuwa na
manager, toka naanza muziki najisimamia mwenyewe.
Tunapata hela za shows
lakini tuna majukumu mengi, mimi natakiwa kula, kuvaa, nilipe kodi
bado kuna familia zinakuangalia. Labda kama kungekuwa na mtu nyuma
ambaye angekuwa anatoa hizo pesa, lakini katika kila pesa ninayoipata
inamahesabu mengi na inanifanya nishindwe kutoa pesa nyingi kwenye vitu
kama hivyo,”
Pia rapper huyo amesema kuna baadhi ya watu walijitokeza kumsimamia
lakini baada ya kukaa nao kwa muda mfupi akaachana nao baada ya kuona
hawawezi kumpatia vitu anavyotaka.
“Kuna watu walijitokeza lakini tulishindwana, unajua hapa nilipo
tayari nimeshafikisha muziki wangu sehemu fulani, unavyokuja kunisimamia
sio kama mtu ambaye una msimamia msanii mchanga, kwa hiyo uje na
mipango iliyokuwa thabiti.
Hapa katikati kuna watu walikuja, siwezi
kuwachoresha lakini ndani ya mwezi mmoja tukashindwana, kwa sababu
mahitaji yangu nayotoka wakawa hawawezi kuyatimiza, tukashindwana, kwa
hiyo kusimamiwa sikatai lakini natama mipango,”
Rapper huyo anajipanga kuachia albamu yake mpya Disemba mwaka huu
baada ya albamu yake iliyopita, ‘Mt Uluguru’ kufanya vizuri kwa kuuza
zaidi ya nakala 9,000.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment