Vanessa Mdee amedai kuwa wakati anasoma shule jijini Paris, Ufaransa
miaka mingi iliyopita wakati familia yake ikiishi huko, alikuwa
akitaniwa na watoto wa kizungu kwakuwa alikuwa na umbo dogo.
Amekumbushia kisa hicho kwenye mahojiano na mtangazaji wa BBC Radio Service , Salim Kikeke kwenye makala ya Kiingereza ya Global Beat: Tanzanian Hip hop.
“Nilikuwa nikitaniwa sana kwasababu nilikuwa mwembamba sana, nilisoma shule Paris na walikuwa wakiniita Msomali,” amesema Vee.
“Nilikuwa nikirudi nyumbani nalia na mama angeniuliza tatizo nini
ningemwambia kilichotokea na unajua kuwa kwenye nchi ya kigeni na
angesema ‘puuzia’ na mimi ningesema ‘unaamisha nini nipuuzie, nataka
uende ukafanye timbwili shuleni’ unajua. Na asingefanya hivyo kamwe,
angeniambia tu ‘puuzia’ sababu hapo ndio moyo wako halisi hujitokeza,
huo ndio wajihi,” alisema Vanessa.
Vanessa anamaanisha kuwa hiyo ndio sababu aliandika wimbo wake Hawajui uliompa tuzo mwaka jana.
Home / News
/ Vanessa Mdee asimulia alivyokuwa akitaniwa utotoni wakati akisoma Paris kutokana na umbo lake dogo
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment