Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Bi. Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
Uteuzi huo umefanyika mwezi huu wa (Desemba 17, 2017) na Kamati ya
Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha waombaji wengine
wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
Vilevile Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya wajumbe katika
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga
atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili
Richard Sinamtwa.
Wajumbe wengine walioongezwa kwenye Kamati hiyo ni Bw. Adam Mihayo na
Bw. Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya
Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Bw. Joseph Mapunda ambaye ameomba
kupumzika.
Pia Bibi Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment