Kocha George Lwandamina amewaandaa viungo Pius Buswita na Raphael Daud kucheza namba nane pacha.
Buswita atacheza namba saba na Daud atacheza namba nane lakini watakuwa wanaweza kupishana.
Uamuzi huo wa Lwandamina unatokana na kuona anamkosa kiungo wake Thabani Kamusoko ambaye ni majeruhi.
“Buswita ni saba na Daud nane, lakini wanaweza kuwa wanabadilishana kulingana na hali ilivyo,” kilieleza chanzo.
“Unajua rotation (mzunguko) itafanya wawe na nafasi ya kupumzika na kushirikiana kulidhibiti eneo la katikati,” alisema.
Inaonekana hali ya Kamusoko haikuwa na uhakika ingawa kuna taarifa kuwa Yanga imekuwa ikifanya siri kuhusiana na kiungo huyo ikitaka awashitukize Simba lakini upande mwingine umeeleza ameshindwa kuripoti kambini Morogoro baada ya kubaki Dar es Salaam akitibiwa.
0 comments:
Post a Comment