NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Mabadiliko Ya Sheria Ya Mwaka 2017 Yaipaisha Sekta Ya Madini


Tito Mselem na Steven Nyamiti, Geita
Imeelezwa kuwa, Sekta ya Madini, imefanikiwa katika usimamizi wake kufuatia mabadiliko ya Sheria yaliyofanywa mwaka 2017 chini ya uongozi wa Rais, John Pombe Magufuli na kuifanya Sekta hiyo kuongoza katika ukuaji kwa asilimia 17.7.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Geita ambapo alisema Sekta ya Madini imeongoza kwa ukuaji kwa asilimia 17.7 na ndiyo Sekta inayoongoza kwa kuiletea Serikali fedha za kigeni.

Waziri Biteko amesema kuwa, Sekta ya Madini inaongoza kwa kusafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi ambapo asilimia 51.9 ya bidhaa zote zinazo safirishwa nje ya nchi zinatokana na Sekta ya Madini.

Vilevile, Waziri Biteko amesema kuwa, mapato yatokanayo na Sekta ya Madini yamepanda kutoka bilioni 168 kwa mwaka mpaka kufikia bilioni 528.

Imeelezwa kuwa ndani ya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kuna kipengele kinachoeleza kuwa kampuni zote zinazo chimba madini nchini Tanzania lazima zifungue akaunti zake ndani ya nchi.

Kampuni ya Barrick iliyoingia ubia na Serikali na kutengeneza kampuni ya pamoja inayoitwa Twiga imefungua akaunti zake zote hapa nchini ambapo mkataba huo ulisainiwa tarehe 24 januari, 2020.

Pia, Waziri Biteko amesema kuwa, Makinikia yanayo safirishwa nje ya nchi yanakuwa yamesha nunuliwa hapa nchini na kuyapima kwenye maabara tatu tofauti ili kujiridhisha kiwango na aina za madini yaliopo kwenye makinikia hayo na fedha zote zinawekwa kwenye banki za hapa nchini tofauti na ilivyokuwa awali.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment