NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

AFANDE SELE AJIBU SUALA LA KIDINI

Msanii wa Hip Hop Afande Sele, ni miongoni mwa wasanii wanaojulikana kuheshimu misimamo yao na kuusimamia vilivyo tamaduni za Kiafrika.  

Ni yeye ndio aliachia ‘kibao’ chake cha ‘dini tumeletewa’, baada ya kushuhudiwa mapigano kadhaa ya wenyewe kwa wenyewe kwa kisingizio cha ‘ukabila’ au ‘dini’.


Na katika wimbo huo alihoji kuwa, kama tusingetawaliwa na Wazungu au Waarabu hizi Dini tungerithi wapi?  tuachane nayo hii nikupeleke kwenye pointi ya msingi.Siku ya leo  staa huyu kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliweka picha akiwa na binti yake kavalia vazi la heshima 

‘Hijab’, akielezea faida zitokanazo na vazi hilo.Sasa shabiki mmoja akamuuliza Afande sele dini yake. “Dini dini? ukishajua itakusaidia nini?” alijibu Afande, Post hiyo haikukaa muda mrefu akaifuta mtandaoni humo.

 

 

 

chanzo>mtembezi

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment