NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

SIMBA YAREJEA KILELEN VPL




MPIRA UMEKWISHAAADAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 87 hadi 90, Simba ndiyo wanaoonekana kushambulia sana kuliko Ndanda ambao wanaanza kucheza kibabe
Dk 86, Msumi wa Ndanda anapiga shuti safi kabisa, linagonga mwamba wa juu wa lango la Simba na kuwa goal kick.

Dk 84, Simba wanaendelea kushambulia, nje ya 18 Awadhi anapiga shuti lakini anabutua juuuuu

Dk 83, Mgosi anawachambua mabeki wawili wa Ndanda na kutoa pasi safi kwa Tshabalala lakini yeye anabutuaa juuu
DK 81 Ponela analazimika kufanya kazi ya ziada na kutoa mpira nje, kona. Inachongwa lakini haina manufaa
SUB Dk 77, Kigi anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Ahmed Msumi upande wa NdandaSUB Dk 75, Kazimoto anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mussa Hassan Mgosi



GOOOOOOOO Dk 72 Kiiza anaifungia Simba bao la tatu, ni baada ya shuti kali la Majabvi, kipa akalitema Lyanga akauwahi mpira na kutoa pasi safi kwa Kiiza
SUB Dk 68, Simba inambadilisha Ajib, anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa Danny Lyanga

Dk 67 Ajib anapewa pasi nzuri kabisa na Awadhi lakini anashinda kuuwahi mpira na Ndanda wanaokoa

Dk 65 KEssy anapiga krosi inakwenda moja kwa moja langoni na kugonga mwamba na kurudi uwanjani, Ndanda wanaokoa
SUB Dk 62 Ndanda wanafanya mabadiliko, Salum Pendeli anaingia kuchukua nafasi ya Mponda
Dk 60, Mponda akiwa katika nafasi nzuri kabisa anapiga shuti kwenye lango la Simba, lakini anashindwa kulenga

GOOOOOOOOOO Dk 57 kona safi ya Ajib, Kiiza anaruka juu kabisa na kupiga kichwa cha kiufundi kabisa na kuandika bao la pili
Dk 56, krosi safi kabisa ndani ya lango la Simba, Atupele anaruka kupiga kichwa lakini anaonekana alifumba macho, anaukosa
Dk 55, Awadhi anaupata mpira wake wa kwanza na kupiga shuti lakini juuu
SUB Dk 54 Awadhi Juma anaingia kuchukua nafasi ya Ndemla
Dk 49 hadi 52, mambo yamebadilika kabisa, Ndanda wanaonekana ndiyo wenye kasi wanawazidi Simba ambao ghafla wanakuwa hawana kasi kabisa

Dk 48, Lufunga anafanya kazi ya ziada na kuokoa krosi ambayo ingemfikia Atupele, basi yangekuwa mengine. Kona safi kabisa ya Kiggi Makasi lakini Simba wanaokoa
Dk 47 Atupele anapokea krosi safi ndani ya 18 lakini anashindwa kuumiliki mpira vizuri na SImba wanaokoa
Dk 46 Brihgson Raphael anaingia kuchukua nafasi ya Omega  Seme

MAPUMZIKO
Dk 41 hadi 45 mpira unaonekana Simba ndiyo wanaoshambulia zaidi lakini Ndanda wanaonekana kuwa makini zaidi
Dk 40 Ntebe anafanya kazi ya ziada, anaokoa mpra mbele ya miguu ya Kiiza inakuwa kona. Simba wanapiga lakini haina manufaaa
Dk 39, Mponda anapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupiga kichwa butu akiwa karibu kabisa ya lango la Yanga
GOOOOOOOO Dk 36, krosi safi ya Kessy, Kazimoro anaunganisha vizuri na kuifungia Simba bao la kwanza

Dk 33, Green anapiga kichwa, kinampita kipa wa Simba, wakati mpira unakwenda kujaa wavuni. Majabvi anaokoa
KADI Dk 31 Ntebe analambwa kadi ya njano kwa kuutupa mpira kwa makusudi
Dk 30, Ntebe anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira na kuwa kona kwenda Ndanda.  Lufunga anapiga kichwa safi lakini mpira unapita juu
Dk 27 krosi safi ya Kazimoto kabla haijamfikia Ndemla, Majabvi anaugusa mpira na kumpoteza maboya mwenzake. Wanapoteza nafasi tena

Dk 26, Kazimoto anajaribu kupiga shuti. Analenga lango lakini ni shuti dhaifu
DK 21 hadi 25, Simba wanaonekana kushambulia zaidi lakini bado inaonekana Ndanda wako makini zaidi katika ulinzi na hakuana hofu hata kidogo.

Dk 19, Kiiza anajaribu kupiga shuti lakini ni dhaifu
DK 17, Ndemla kwa mara nyingine anapiga shuti lakini anashindwa kulenga
Dk 15, Simba wanafanya shambulizi tena, krosi safi ya Ajib, Kiiza naye anampasia Kessy, anapiga krosi safi hata hivyo Ndanda wanaokaoa
Dk 12, Ndemla anaingia vizuri na kupiga shuti kali lakini linapita juu kidogo ya lango
Dk 9, Majabvi anapiga shuti lakini linakuwa dhaifu na halilengi lango
Dk 7, Tshabalala anapiga krosi lakini inaonekana kuwa dhaifu, kipa anadaka kwa ulaini. Mechi inaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 4, Atupele Green anajaribu kupiga shuti, lakini anabutua kabisa
Dk 1, mechi inaanza taratibu kila upande ukionekana kuusoma mwingine kwa umakini
 



 
 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment