Taasisi ya kuzuia na kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inamshikilia ofisa kodi msaidizi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Flavian Chacha kwa
makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya sh. 1.5 milion kutoka kwa
mfanyabiashara wa matofali.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake , mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga amesema
kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na TAKUKURU baada ya mfanyabiashara
aliyefahamika kwa jina la Jackson Shirima kwenda kutoa taarifa za
kuombwa rushwa na Ofisa huyo.
Kuhangwa amesema kuwa Ofisa huyo
aliomba rushwa ya sh. 1.5 milioni kwa mfanyabiashara huyo ili
asimchukulie hatua kwa kosa la kusafirisha mzigo wa matofali bila kutoa
stakabadhi ya mauzo.
Amesema mtuhumiwa ametenda kosa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Amesema Machi 18 mwaka huu maofisa wa
TRA wakiwa katika shughuli zao za kikazi walilikamata lori aina ya
Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na Joshua Charles likiwa na
mzigo wa matofali kutoka kiwandani kwa Shirima, ambapo baada ya
kulikagua walibaini kwamba mali hiyo iliuzwa bila kutoa stakabadhi,
hivyo walimwamuru dereva wa gari hilo kulipeleka ofisi za TRA kwa hatua
zaidi.
Amebainisha kuwa baada ya gari hilo
kukamatwa, dereva wa gari hilo alimpigia simu tajiri wake (Shirima) ili
alete stakabadhi iliyokuwa inadaiwa na maofisa wa TRA.
Ameongeza kuwa baada ya mazungumzo
marefu kati ya Shirima na Ofisa wa TRA (Chacha), ndipo alipomweleza
Shirima atoe faini ya sh. 3 milion ambapo baada ya kuomba sana ndipo
alipopunguziwa hadi sh 1.5 milioni ndipo alipoomba nafasi ya kwenda
kuzitafuta fedha hizo.
Kwa upande wake Jackson Shirima amesema
kuwa baada ya kuombwa kiasi hicho cha fedha aliamua kwenda moja kwa
moja kwenye ofisi za TAKUKURU mkoa wa Dodoma na kutoa taarifa za tukio
hilo ambapo baada ya kujiridhisha kuwa kulikuwa na viashiria vya rushwa
mtego uliandaliwa na kufanikiwa kumtia ofisa huyo mbaroni.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
AFISA TRA KIKAANGONI KWA KUPOKEA RUSHWA YA MILIONI 1.5
Reviewed by Newspointtz
on
11:48:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment