NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPATIKANA LEO MACHI 22, 2016

Dar es salaamHalmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilitangaza Machi 22 kuwa ndiyo kitafanyika kikao cha Baraza la Madiwani wa Dar es Salaam kujadili ajenda moja ya uchaguzi wa meya.

Uchaguzi huo uliahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM, katika Mahakama Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene hivi karibuni, alisema zuio hilo ni batili na kuagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya uchaguzi huo kabla ya Machi 25.

Machi 15, Mwaka huu, Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana alithibitisha kuwa uchaguzi huo utafanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee.

Alisema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ikiwamo kusambaza barua kwa viongozi wa vyama husika na wajumbe watakaoshiriki kikao hicho.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli jana aliagiza pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika leo tarehe 22 Machi, 2016 badala ya kuendelea kurumbana.

“Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli aliongeza Rais Magufuli

 

chanzo>mtembezi

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment