Ray
Tomlinson, raia wa Marekani, ambaye ndiye aliyevumbua utumiaji wa barua
pepe kwa Kiingereza e-mail amefariki dunia mvumbuzi huyo amefariki akiwa
na umri wa miaka 74.
Mgunduzi huyu aliibuka na wazo la kutuma
ujumbe wa kieletroniki kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia mitandao
mbali mbali mwaka 1971 huku historia ikieleza kuwa aliandika ujumbe wa
kwanza wa barua pepe wakati akifanya kazi Boston, kama Mhandisi wa
kompyuta.
Pia alikuwa mwanzilishi wa matumizi ya
alama “at”(@)kuwa ndio alama kuu ya utumaji wa barua pepe, ikikumbukwa
kuwa wakati wa uhai wake Tomlinson alisema hawezi kukumbuka barua pepe
yake ya kwanza ilielezea nini.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
ALIYEGUNDUA BARUA PEPE AFARIKI DUNIA
Reviewed by Newspointtz
on
17:30:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment