Serikali
kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamewapongeza
wasanii wa Tanzania kwa kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania nje ya
mipaka kwa kufanya vizuri na kuibuka na ushindi ikiwemo tuzo katika
filamu bora za Kiswahili zinazotoka Tanzania.
Akitoa pongezi hizo mapema leo 7 Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na wasanii mbalimbali wa filamu nchini waliowasindikiza washindi wa tuzo hizo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,
Akiwemo mshaindi wa tuzo ya filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language -Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’, Msanii Single Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri aliwapongeza kwa mshikamano wao huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa pongezi.
Waziri Nape amebainisha kuwa, awali Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria, alipata Baraka kutoka kwake hivyo hata kurejea kutoa shukrani ni jambo jema huku akieleza kuwa, Serikali itahakikisha inawalea wasanii katika umoja pamoja na kuweka mazingira mazuri ya ufanisi katika shughuli zao ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na misingi ya sharia katika kuifanya tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kuleta fursa za ajira kwa wasanii ndani na nje.
“Kwa nafasi yangu ya Uwaziri. Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia malengo tuliyoyakusudia. Hii ni paamoja na kuwa na Sera madhubuti na kuzuia mianya ya wafujaji wa kazi za Wasanii wa Tanzania.
Serikali ya awamu ya tano kupitia kwa Rais wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza na ili la stika za TRA na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya Mapato inavyopambana na watu wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa kufunga maduka yao huu ni mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili” alieleza Mh.Nape na kupaata pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao waliweza kushangilia kwa kauli hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.
Aidha, katika tukio hilo, Serikali imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda tuzo hizo za AMVCA 2016 vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na wasanii wote ambao filamu zao pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na waandaaji waliowezesha filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.
Katika tuzo hizo mbali na Rich Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine aliyeshinda ni pamoja na Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’.
Katibu
wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso
akiwatambulisha wasanii kwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na
Michezo, Nape Nnauye (kulia) wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi
Msanii
wa filamu ya Shoe Shine na Samaki Mchangani, Amri Shivji akitoa
shukrani zake kwa Serikali. Shivji naye filamu yake ya Samaki Mchangani
iliweza kushiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016, kama filamu ya
Kiswahili.
Msanii
Single Mtambalike ‘Rich Rich’ akizungumza machache juu ya ushindi wake
ambapo pia ameipongeza Serikali kwa ushirikiano waliowapa hadi kufikia
hapo.
Msanii wa filamu ambaye naye filamu yake ilishiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016 akitoa shukrani zake kwa Serikali
Waziri
wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati)
akizungumza juu ya kuwapongeza wasanii Rich Rich na Lulu Michael kwa
ushindi wao katika tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika nchini Nigeria
mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa Wizara hiyo.. Mapema leo 7
Machi.2016
Mkutano huo ukiendelea…
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti maalum cha pongezi, Msanii wa filamu Amir Shivji
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akitoa vyeti kwa wasanii waliofanya vizuri.
Waziri
wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti
cha pongezi Joseph Lukaza Mwakilishi wa Proin akipokea cheti kwa niaba
ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye bado hajarudi kutoka Nchini
Nigeria.
Waziri
wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti
Msanii Rich Rich kama pongezi kwa Serikali. Kulia anayeshuhudia ni
Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce
Fisso wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi.2016
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akipokea tuzo hiyo kutoka kwa msanii Rich Rich.
Waziri
wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa amebeba tuzo
hiyo kama ishara ya kuwawakilisha watanzania wote.
Waziri
wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye na Msanii Rich
Rich (katikati ) wakiwa katika picha ya pamoja wasanii wengine na
viongozi wa Wizara hiyo.
Katibu
wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso
akipiga picha ya ukumbusho na Msanii Rich Rich wakati wa mkutano huo
mapema leo 7 Machi.2016. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Akitoa pongezi hizo mapema leo 7 Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na wasanii mbalimbali wa filamu nchini waliowasindikiza washindi wa tuzo hizo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,
Akiwemo mshaindi wa tuzo ya filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language -Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’, Msanii Single Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri aliwapongeza kwa mshikamano wao huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa pongezi.
Waziri Nape amebainisha kuwa, awali Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria, alipata Baraka kutoka kwake hivyo hata kurejea kutoa shukrani ni jambo jema huku akieleza kuwa, Serikali itahakikisha inawalea wasanii katika umoja pamoja na kuweka mazingira mazuri ya ufanisi katika shughuli zao ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na misingi ya sharia katika kuifanya tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kuleta fursa za ajira kwa wasanii ndani na nje.
“Kwa nafasi yangu ya Uwaziri. Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia malengo tuliyoyakusudia. Hii ni paamoja na kuwa na Sera madhubuti na kuzuia mianya ya wafujaji wa kazi za Wasanii wa Tanzania.
Serikali ya awamu ya tano kupitia kwa Rais wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza na ili la stika za TRA na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya Mapato inavyopambana na watu wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa kufunga maduka yao huu ni mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili” alieleza Mh.Nape na kupaata pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao waliweza kushangilia kwa kauli hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.
Aidha, katika tukio hilo, Serikali imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda tuzo hizo za AMVCA 2016 vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na wasanii wote ambao filamu zao pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na waandaaji waliowezesha filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.
Katika tuzo hizo mbali na Rich Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine aliyeshinda ni pamoja na Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’.

0 comments:
Post a Comment