NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

BAADA YA KUICHAPA APR,YANGA MIKONONI MWA AL AHLY YA MISRI


Al Ahly wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Fc Libolo ya Angola katika mchezo wa pili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali inayothibitisha rasmi kuwa wababe hao kutoka Misri watakwaana na Yanga katika mchezo ujao wa michuano hiyo

 Yanga imeitoa APR kwa mbinde kwa jumla ya mabao 3-2, sasa inakutana tena na Al Ahly waliowatoa katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.

Katika mechi hiyo, Al Ahly ilianza kupata bao lake katika dakika ya 10 Sobhy likadumu hadi mapumziko na kipindi cha pili ikafunga bao la pili kupitia Antui aliyemaliza kazi katika dakika ya 83.

Wakati wanaitoa Yanga, Ahly walionekana kuwa wachovu, kwani walilazimika kuwang’oa Yanga kwa mbinde wakiwa chini ya Kocha Hans van der Pluijm.

Pluijm  aliingoza Yanga kuitwanga Ahly bao 1-0 jijini Dar es Salaam, iliposafiri hadi Alexandria, Yanga ikafungwa bao 1-0. Wakaingia kwenye mikwaju ya penalti, ikang’oka.

Mbuyu Twite na Said Bahanuzi ndiyo waliopoteza penalti kwenye Uwanja wa Jeshi wa jijini Alexandria.

chanzo>mtembezi

 

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment