08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba.07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Hapa
chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa
na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi
unaoendelea Zanzibar.
Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu
waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka
Ulaya ambao hawakuwa na habari.
07:44 Usalama umeimarishwa
visiwani. Hapa chini ni maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa
kabla ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Unguja.
07:42 Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba.
07:30 Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.
Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi.
07:20 Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein, mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura Unguja.
07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja. 07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa. 06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo. Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri. 06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe.
06:35 Katika vituo vingi, wapiga
kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na
maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.
06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani
Zanzibar wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo ya
uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi.
Chama cha CUF kinasusia uchaguzi huo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi huo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Uchaguzi wa marudio Zanzibar
Reviewed by Newspointtz
on
08:18:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment