Bus dogo aina ya Toyota Hiace lililokuwa linatoa huduma ya kubeba wanafunzi ya Shule ya Southern Medium Education Centre ya Mjini Newala Mkoani Mtwara limeteketea kwa moto jioni ya leo tarehe 17 2016 likiwa limeegeshwa shuleni hapo mtaa wa Nangwala Chini.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni baada ya kuwarudisha wanafunzi makwao na kurudi kuengeshwa shuleni hapo na chanzo cha moto huo hakijafahamika lakini taarifa zilipata chadonews baada ya kufika eneo la tukio na mashuhuda kwa sharti la kutotajwa jina wamedai moto huo ulianzia kwenye injini.
“Gari ilikuwa imepack ghafla tukaona Moshi mzito unatoka kwenye injini kulikuwa na watu wakaanza kuzima kwa kutumia maji ila ikawa kama wanaongeza baadae wakaanza kuzima kwa mchanga lakini ukawashinda wakaamua kuacha na hali ndio kama unavyoiona” alieleza mmoja wa mashuhuda hao.
Polisi waliofika eneo la tukio kusaidia kuokoa walikuta gari hiyo ikiwa imeteketea kabisa hata hivyo jeshi hilo halikuwa tayari kuzungumza lolote mpaka watakapopata taarifa za kiuchunguzi wa tukio hilo. Katika tukio hilo hakuna majeruhi wa kifo. Chadonews inawapa pole waliofikwa na tukio hilo la kusikitisha.
chanzo>chadonews
0 comments:
Post a Comment