NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Mahakama Yataka Upelelezi wa Kesi Ya Wabunge Halima Mdee, Mwita Waitara na Saed Kubenea Ukamilike Haraka


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili kesi inayowakabili wabunge watatu wanaotokana na Ukawa na madiwani wao ianze kusikilizwa.

Washtakiwa hao ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mwita Waitara (Ukonga) na Saed Kubenea (Ubungo).

Madiwani wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Ephrein Kinyafu (Kimara), Manase Njema (Kimanga, Tabata) na kada wa chama hicho, Rafii Juma.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa kauli hiyo jana baada ya Wakili wa Serikali, Mbunito Aloyce kudai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.

Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliuomba upande wa mashtaka kuanza kuisikiliza kesi hiyo kwa sababu washtakiwa walikamatwa haraka haraka na usikilizaji wake uwe vivyo hivyo.

Washtakiwa hao wanaodaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando katika vurugu zilizotokea Februari 27,2016 Ukumbi wa Karimjee kwenye Uchaguzi wa meya na naibu meya wa jiji la Dar es Salaam, wanatetewa na Mawakili Peter Kibatala na John Malya. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18.
chanzo?mpekuzi
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment