NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Bulaya Akamatwa na Polisi usiku wa Kuamkia leo


 Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi  jijini Mwanza na kulazimika  kulala  rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha  kumpeleka  kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya. 
Wabunge hawa pamoja  na  uongozi  wa  juu  wa  CHADEMA  Wako  jijini  Mwanza  kwa  ajili  ya  kikao  cha Baraza  Kuu  la  chama  hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest
 
 
 
 
chanzo>mpekuzi 
 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment