Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi
Gerson Lwenge ameiagiza bodi ya kampuni ya maji safi na taka Dar es
salaam (DAWASCO kuwasimamisha kazi watendaji tisa wa mamlaka hiyo pamoja
na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Injinia Jackson Midalla
kupisha uchunguzi uliosababisha hasara ya kiasi cha shilingi bilioni.2.9
ambazo kampuni ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka Strabag
ilipaswa kulipa.
Agizo hilo limetolewa jijini Dar es
salaam na Mhandisi Lwenge alipokuwa akizungumza na watendaji wa DAWASCO
ofisini kwao ambapo amesema katika uchunguzi wa awali, imeonekana kiasi
hicho cha fedha kilitakiwa kulipwa na kampuni ya stragbag kwa ajili ya
matumizi ya maji katika ujenzi wa barabara lakini hazijaingia na kubaini
kuwa wapo baadhi ya watendaji waliohusika kwa namna moja ama nyingine
katika suala hilo.
Mhandisi Lwenge amewataja watendaji hao
ambao wanatakiwa kusimamishwa kazi mara moja na kutafutwa popote alipo
aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo injinia Jackson Midalla wakati
huo.
Aidha, ameitaka bodi hiyo kufanya
uchunguzi wa haraka na kuhakikisha kampuni ya strabag inalipa kiasi
hicho cha fedha ndani ya siku 14 vinginevyo hatua za kisheria zitafuata
na kufuatilia akaunti za makampuni na viwanda vikubwa ili kujiridhisha
kama zinalipia huduma ya maji.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Waziri wa maji atumbua jipu LA DAWASCO
Reviewed by Newspointtz
on
10:54:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment