NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

CAF YATANGAZA KUIONDOA CHAD, YAPIGA FAINI YA SH MILIONI 44


Shirikisho la Soka Africa (Caf), limetangaza kuiondoa Chad katika michuano ijayo kuwania kufuzu kucheza Afcon na mingine yote iliyo chini yake.

Kama hiyo haitoshi, Caf imetangaza kuitwanga Chad faini ya dolla 20,000 (zaidi ya Sh milioni 44) kutokana na kitendo chake cha kujiondoa katika michuano ya ya kuwania kucheza Afcon.


Chad ilitarajiwa kucheza kesho dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuwa imetwangwa bao 1-0 kwao ND’jamena
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment