newspointtz blog
Benki
ya CRDB imemfungulia Akaunti ya Scholarship na kumwekea sh.
Milioni 5 mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa
kumaliza kidato cha nne mwaka 2015, Butogwa Shija na kumwahidi
ajira pindi amalizapo masomo.
Hafla
hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea
kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo, ambapo
Butogwa alipewa zawadi ili kuwahamasisha watoto wa kike kwamba
wanaweza.
Pia
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilimuongezea mwanafunzi huyo
kiasi cha shilingi 500,000 lengo likiwa ni kuwahamasisha watoto
wa kike ili kuleta haki sawa kwa wote.
Naye
Butogwa aliahidi kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa
bidii bila kubweteka na kuwataka wanafunzi wengine kuweka bidii
kwenye masomo yao.
Katika
hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Esther Kitoka
alisema wametoa sh. milioni 20 zitakazosaidia katika ujenzi wa
mabweni kwa watoto wa kike ili kuongeza kasi ya ufaulu kwa
wanafunzi
chanzo>
0 comments:
Post a Comment