Baada ya kudumu Ikulu kwa takribani
siku 127 zikiwamo 67 tangu aongezewe muda wa mwaka moja akiwa na
Serikali ya Awamu ya Tano, Balozi Ombeni Sefue ameshukuru heshima
aliyopewa na Rais John Magufuli kwa muda wote aliomsaidia kutekeleza
majukumu yake ya ukatibu mkuu kiongozi na kueleza kuwa Serikali ya sasa
ni ya mabadiliko.
Wakati Sefue akiondoka, mhandisi John
Kijazi amepokea kijiti cha ukuu wa utumishi serikalini na kuahidi kuwa
atafuatilia mazingira ya watumishi wote pamoja na mazingira yao, ili
kurekebisha panapohitajika kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na tija kwa
wananchi.
Akizungumza muda mfupi baada ya
kuapishwa kwa mrithi wake, licha ya kumshukuru Rais, Balozi Sefue
aliwataka watendaji wote serikalini kumpa ushirikiano wa kutosha Balozi
Kijazi ili kuleta ufanisi kwenye huduma za umma.
“Namshukuru Rais kwa
kuniamini kwa kipindi chote nilichodumu naye. Ni heshima kubwa
kuwatumikia Watanzania pamoja naye. Nitampa ushirikiano wowote
atakaouhitaji katibu mkuu kiongozi mpya kwenye utekelezaji wa majukumu
yake,” alisema Sefue.
Rais Magufuli, ameahidi na mara zote
amekuwa akisisitiza adhma yake ya kutumbua majipu kwa watumishi wote
ambao hawaendani na kasi yake.
Tangu taarifa za mabadilio hayo
zilipotangazwa jana, kumekuwepo na tetesi nyingi kuwa huenda Sefue naye
ni jipu lilikuwepo ikulu, suala ambalo halikupata maelezo ya kutosha
kutoka kwa balozi huyo.
Alipoulizwa juu ya tetesi hizo alijibu kwa ufupi: “Hii ni Serikali ya mabadiliko.”
Kwa upande wake Kijazi, alisema
atafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Rais huku akimshauri namna
sahihi za kuboresha mazingira ya utumishi serikalini.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
SEFUE ASEMA NENO BAADA YA KUENGULIWA IKULU
Reviewed by Newspointtz
on
08:23:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment