Baada
ya rapa Chidi Benz kuomba msaada ili asaidiwe kuirudisha afya yake
ambayo imethorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevyana na
baadae kusaidiwa na Babu Tale kwa kupelekwa rehab.
Wadau mbalimbali pamoja na wasanii wenzake walimpongeza Babutale lakini Dudu Baya amedai hakupenda rapa huyo asaidiwe.
Akizungumza
na Bongo5 Jumamosi hii, Dudu amedai rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa
ndio maana baada ya kusaidiwa anataka kujipangia baadhi ya mambo.
“Watu
mfano wa Chidi Benz hawatakiwi kusaidiwa, niwakuachwa wafe na wazikwe.
Kwanza ni waongo, ukikutana nao utasikia naumwa au nimefiwa, utampa
msaada, mwisho wa siku anaenda kujidunga. Misaada kama hii inatufanya
majina yetu kuwekwa kataka orodha ya wauaji (killers),” alisema Dudu.
Aliongeza,
“Babutale na wenzake walipomfisha Chidi Benz rehab kwanza alianza
kuweka masharti yake kituoni, mara hawezi kushauriwa na mtu ambaye
hajawahi kutumia sumu hiyo (unga).
Hapo
ndipo nilipogundua amebebwa kinguvu bila yeye kuwa tayari kupona. Ni
sawa na mgonjwa apelekwe hospitali then aanze kutoa masharti yake,
eti hiki kitanda sikitaki. Wewe dokta huwezi kunitibu kwa sababu
hujawahi kuumwa ugonjwa ninaoumwa, mgonjwa kama huyo si nachotaka ni
kifo?.
Hata
wakati yesu amekuja kutukomboa na dhambi, aliponya wagonjwa waliokuwa
tayari kupona, hata leo umpeleke ndugu yako kanisani au msikitini
akaombewe aache ulevi au umalaya, kama hana dhamira ndani ya moyo wake
ya kuacha, hakiwezi tokea chochote,”
Pia Dudu amesema wasanii wengi wanasikia kila siku kuhusu madhara ya Madawa ya kulevya lakini wanapuuzia.
“Chidi
Benz si mtoto mdogo, ameshuhudia wasanii na watu wa kawaida wengi
tukiwapoteza kwa sababu ya Madawa ya kulevya lakini wanapuumzia,
wanarudia kubwia tena.
iweje
leo yeye ajiingize kataka ulimwengu huo? hakika kifo anakitaka mwenyewe
na si kurubuniwa. Uzuri wa Tanzania hatuna umasikini wa ardhi, watu
kama hawa hawana faida kwa taifa, niwakuacha wafe na wazikwe.
Na
kama inawezekana Mh Rais Magufuli angetoa amri mateja wakifa wazikwe na
jiji. Kwa sababu sioni ndugu yeyote wa Chidi yuko bize na rapper
huyo.
Kwanini
nyingi mumpaparikie au ndio mnauchukungu kuliko ndugu zake?.
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu,” alisema Dudu.
0 comments:
Post a Comment