Beki wa Sunderland, Emannuel Eboue amefungiwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kujihusisha na soka kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na kutokea mzozo wa mkataba kati yake na wakala wake za zamani, Sebastien Boisseau.
Aidha katika taarifa imeyotolewa na FIFA imeeleza kuwa mchezaji huyo kabla ya kurudi katika soka anatakiwa kumlipa wakala wake wa zamani CHF 30,000 ambayo kwa Tanzania sio chini ya Mil. 68.
“Kamati ya Maadili ya FIFA imempa adhabu Mr. Eboue pamoja na faini ya CHF 30,000 kwa kushindwa kuzingatia sheria za wachezaji kwa kuvunja Kifungu 64 cha Kanuni za maadili ya FIFA,
“Pia mchezaji anapewa muda wa neema wa siku 120 kukaa na wakili wake wa zamani, Mr. Boisseau na kumaliza tofauti zao kama itashindikana Mr. Eboue atapewa adhabu ya kutokujihusisha na shughuli yoyote ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja,”
Aidha klabu yake ya Sunderland inataraji kumwandikia barua ya kusimamisha mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.