MJUKUU
wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume,
amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais
Visiwani, anaandika Pendo Omary.
Fatma
Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume
amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa
madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”
Amesema,
“Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi.
Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa
rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”
Akiongea
kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini
kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi,
kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo
utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”
Amesema,
“CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi
wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”
Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment