NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Ferguson ataja club inayoweza kuizuia Leicester kwenye ubingwa.




fer
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameongoea na Sky Sport kuhusu mbio za ubingwa msimu huu kwa jinsi ulivyo sasa hivi.

Kocha Ferguson ameshinda mataji 13 kwenye muda wa miaka 26 aliyokaa ndani ya Old Trafford, hivyo maneno yake kuhusu chochote cha EPL lazima kichukuliwe serious.

Sir Ferguson anasema Tottenham Hotspurs ndio timu pekee yenye uwezo wa kuizuia Leicester City kwenye mbio za ubingwa. Ferguson amesema “Leicester wanakaribia kwenye mstari wa kumaliza kama mabingwa, hiyo ni task kubwa sana kwao.

 Wanatakiwa kuwa hivi hivi hadi mwisho na hawatakiwi kibadirika, wanatakiwa kuwa hivi hivi kama walivyokua kwa miezi 6 iliyopita”.

“Naiona Spurs pekee kuwa ni ya hatari kwa Leicester City. Spurs kwa sasa wanacheza soka zuri
 zaidi ya miaka mingi niliowajua kwa miaka kadhaa iliyopita. Leicester wamekua timu bora kwa msimu mzima na wanastahili kushinda ubingwa.”
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment