NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

HUDUMA BORA ZA AFYA ZAIPAISHA TANZANIA KIMATAIFA

 

Tanzania inaongoza miongoni mwa nchi 15 za kiafrika katika mradi wa utoaji wa huduma bora za Afya kwa jamii,Mazingira ya kufanyia kazi na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wagonjwa unaofadhiliwa na shirika la misaada la kimataifa la Japan (JICA).

Mkufunzi wa kitaifa wa mradi huo unaojulikana kama 5 s Bi.Salome Saria amesema,tathimini iliyofanywa na makao makuu ya JICA baada ya miaka kumi ya utekelezaji tanzania imeonekana kufanya vizuri zaidi kati ya nchi hizo.

Bi Saria amesema hayo katika taarifa yake kwa maafisa wa JICA Tanzania wanaofuatilia utekelezaji wa mradi huo katika Hospitali ya rufaa ya KCMC ambao sasa umeanza kutoa huduma  katika vyuo vikuu ya tiba vilivyopo KCMC na maendeo mengine nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya  mradi huo Dkt.Mosi Mwasamwaja ameyataja baadhi ya mafanikio ya mradi kuwa ni pamoja na usalama wa wagonjwa ukiwemo upatikanaji wa dawa, ukuboresha mazingira ya kufanyia kazi, kupunguza kero za wafanyakazi na kuondoa mtazamo chanya wa kulaumu uongozi.

Mradi wa mradi huo kutoka ofisi ya JICA Tanzania Bi Christine Shirima amesema, wameamua kusaidia mradi huo unaosimamiwa na wizara ya afya ili kuboresha huduma za afya kwa wafanyakazi wa Tanzania na nchi nyingine za Kiafrika.

 chanzo>mtembezi

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment