Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto
Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba
atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika
Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka
2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa
mchanga kwa bandari ya Kigoma.Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini
Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini
kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo
hazikuwa sahihi.
Zitto alisema Rais Kikwete alipewa
taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo
unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya
Kigoma.
Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema
kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kupanuliwa
kwa Mto Lukuga kunafanya maji kutoka kwa wingi na kuingia bahari ya
Atlantiki ndiko kulikochangia kupunguza kina cha maji katika maeneo
mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa
mwaka 2008 inaonyesha kuwa kiasi cha Sh bilioni tano kilikuwa
kikihitajika kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi hao, fedha ambazo
uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imesema haiwezi
kuzilipa hivyo kutaka mamlaka za serikali kuona namna ya kutafuta fedha
hizo na kugharamia kuwalipa watu hao.
Wakizungumzia kauli ya Zitto, baadhi ya
wakazi wa eneo la Mlole ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na agizo
hilo la Rais Kikwete, walisema kuwa wameanza kupata matumaini ya kuona
thamani ya nyumba zao kwani tangu kutolewa kwa agizo hilo nyumba zao
zimekuwa hazina thamani mahali popote.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
ZITTO: AGIZO HILI LA KIKWETE LI TENGULIWE
Reviewed by Newspointtz
on
08:58:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment