SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema
Bunge la Tanzania litaendelea kuimarisha na kukuza ushirikiano na Bunge
la Vietnam, ikiwa ni muendelezo wa uhusiano nzuri ulipo baina ya mataifa
hayo mawili.
Ndugai aliyasema hayo jana jijini Dar
es Salaam wakati akizungumza na waandishi habari, muda mfupi baada ya
kufanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Troung Tang Sang anayeondoka
nchini leo, baada ya kumaliza ziara yake ya siku nne hapa nchini.
Alisema Tanzania imekuwa na uhusiano
mzuri na Vietnam kwa muda mrefu na kwamba mwaka 2009 wabunge wa Tanzania
walitembelea Bunge la Vietnam. Pia mwaka 2011 wabunge wa nchi hiyo nao
walitembelea Bunge la Tanzania na kufanikiwa kubadilisha uzoefu wa
mabunge yao.
Ndugai alisema kupitia uongozi wake
atahakikisha uhusiano unakuwa endelevu kwa faida ya nchi na Watanzania
wote. “Rais wa Vietnam na mimi tumekubaliana kushirikiana katika masuala
mbalimbali ya Bunge, ukuzaji uchumi na biashara na kuimarisha uhusiano
wa mabunge yetu zaidi,” alisema.
Katika mazungumzo, Ndugai aliongozana
na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge,
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Hawa Ghasia, Mwenyekiti wa Kamati ya
Kilimo, Mifugo na Maji na Mbunge wa Segerea Bonnah Kalua ambaye ni
Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Leo Rais huyo
anaondoka nchini kwenda Msumbiji kwa ziara ya kikazi.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
HUU NDIO MKAKATI WA BUNGE LA TANZANIA NA LA VIETNAM
Reviewed by Newspointtz
on
11:36:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment